New Book Release! UJUMBE WA MALAIKA WATATU UMASAINI: Maisha na Utume wa Dkt. John Aza Kisaka

Ujumbe wa Malaika Watatu Umasaini: Maisha na Utume wa Dkt. John Aza Kisaka, si wasifu wa Dkt. John Aza Kisaka, bali ni kisa cha utume wa Kiadventista Umasaini kikisimulia huduma ya zaidi ya miaka arobaini ya Dkt. Kisaka kwa jamii ya Wamasai. Simulizi hii ya kusisimua, inaangazia kazi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Umasaini, kupitia huduma ya upendo na kujitoa ya Dkt. Kisaka tangu alipowasili huko kwa mara ya kwanza mwaka 1964. Kitabu kimeandikwa kama simumilizi, kwa lugha rahisi ili kumwezesha kila mtu kusoma, kujifunza na kufurahia mbinu na njia mbalimbali za kupeleka ujumbe wa Malaika Watatu katika maeneo mapya au kwa jamii ambayo bado haimjui Mungu pekee wa kweli na Yesu Kristo aliyemtuma. Katika kitabu hiki, msomaji atajifunza jinsi Mungu alivyobadilisha maisha ya watu wengi na kuleta upataniisho kati ya makabila mawili yaliyokuwa maadui wa jadi, yaani Wapare na Wamasai. Msomaji atafurahi pia kujua kwamba, kupitia kwa Injili, Mungu anaokoa, anaponya, na anarejesha.

Buy it now on Amazon at https://a.co/d/0d1mdT57

Scroll to Top